1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhoruba na pepo kali zapiga Kaskazini Magharibi ya Marekani.

17 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CBI2

Seattle:

Dhoruba na pepo kali zilizopiga kaskazini magharibi ya Marekani zimsesababisha si chini ya watu wanne kufa. Kwa muda fulani zaidi ya watu milioni moja walibakia bila ya umeme katika mkoa wa Washington. Wakuu walitangaza hali ya hatari. Kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa, pepo na dhoruba hizo kali zitapungua leo. Ilitajwa kwamba kasi za pepo zilifikia mwendo wa kilomita 144 kwa saa.