1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Didier Drogba ameumia,Essien azika ndoto ya kucheza Kombe la dunia.

4 Juni 2010

Ujerumani bila Ballack safari ya Afrika Kusini Jumapili hii:

https://p.dw.com/p/NiUr
Drogba ameumia.Picha: picture-alliance/dpa

Baada ya Brazil, mabingwa wa dunia mara 5 kuifunza Zimbabwe, darasa la dimba kwa kuitandika mabao 3:0, keshokutwa Jumatatu ni zamu ya Taifa Stars,Tanzania kuikaribisha Brazil,mjini Dar-es-salaam. Je, mashabiki wa Tanzania wasemaje ?

Kocha wa Ujerumani,Joachim Löw ,anafunga safari kesho Jumapili na timu yake ya chipuklizi kuelekea Afrika Kusini.

Na je, mzee Nelson Mandela, atahudhuria ufunguzi wa Kombe la dunia hapo Juni 11 pale Bafana Bafana, itakapofungua dimba na Mexico huko City Stadium,Johannesberg ? Didier Driogba nae ameumia akicheza na Japan.

Macho ya mashabiki wa dimba sio tu nchini Tanzania, bali Afrika Mashariki na Kati kwa jumla, yanakodolewa mpambano wa keshokutwa Jumatatu kati ya Brazil na Taifa Stars. Brazil hapo kabla iliikomea Zimbabwe mabao 3:0.

Wakati watanzania wanafurahia kutembelewa na akina Kaka na Robinho, gharama za kuileta Brazil,Tanzania za hadi Tsh. Bilioni 1, zimezusha mjadala motomoto. miongoni mwa mashabiki na wasio mashabiki.

Ujerumani, chini ya nahodha wake mpya Philipp Lahm, itafunga safari Jumapili hii kuelekea Afrika kusini,ambako Juni 13, itafungua dimba katika kundi D na Australia,mjini Durban.

Juni 23,Ujerumani, ina miadi na Black Stars -Ghana.

Mpambano ambao utapunmgwa na shetani wa mghana Kevin Prince Boeteng,aliemtimba na kumuumiza nahodha wa Ujerumani Michael Ballack,mwezi uliopita wakati wa finali ya Kombe la FA kati ya Chelsea na Portsmouth.

Kocha Löw,anaweka nyuma misukosuko ya hivi karibuni ya kuumia Michael Ballack, mchezaji wa kiungo Christian Traesch na mlinzi Heiko Westermann. Kocha Löw, anatumai kikosi chake cha chipukizi kama Mesut Oezil,Marko Marin,Lukas Podolski,chini ya nahodha Philipp Lahm, kitazusha maajabu Afrika kusini kuanzia wiki ijayo.

Na huko Afrika Kusini kwenyewe,swali limekuwa likiulizwa:Je, mzee Mandela, mwenye umri wa miaka 91 na aliechangia sana kulileta Kombe la Dunia Afrika Kusini, atahudhuria dimba la ufunguzi Ijumaa ijayo ?

Familia yake inasema kwamba, mzee Mandela, afya yake haimruhusu lakini ,gazeti moja la Afrika Kusini, limefichua kuwa mzee Mandela, atakuwa uwanjani siku hiyo ya ufunguzi.

Taarifa za hivi punde zasema kwamba, stadi wa Ivory Coast na Chelsea , Didier Drogba ameumia kisugudi.Swali ni je, atakuwa fit kuiwakilisha Ivory Coast katika Kombe lijalo la dunia ? Au atafuata nae nyayo ya akina Michael Essie wa Ghana na Michael Ballack wa Ujerumani ?Wote ni mastadi wa Chelsea.

Mwandishi: Ramadhan Ali/AFPE/DPAE

Imepitiwa na :Hamidou Oummilkheir