1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Diego Maradona amefariki dunia

Josephat Charo
25 Novemba 2020

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 60. Maradona alikuwa akisumbuliwa na maradhi katika siku za hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/3lpO2
Diego Maradona File Photo
Picha: Martin Rickett/PA/picture alliance

Gwiji la soka raia wa Argentina Diego Maradona amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 60, msemaji wake ametangaza Jumatano.

Mapema mwezi huu, Maradona aliondoka hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa damu iliyokuwa imeganda katika ubongo wake, huku wakili wake Matias Moria akisema ulikuwa muujiza kwamba damu hiyo iliyoganda, ambayo ingesababisha kifo chake, ilikuwa imegundulika mapema.

Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, Maradona amelazwa hospitali mara tatu kwa hali mbaya ya afya kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya na kilevi. Hivi karibuni, alilazimika kukaa karantini nyumbani kutokana na janga la COVID-19.