1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dimba la AFCON laingia nusu fainali

Bruce Amani
30 Januari 2017

Misri imekuwa timu ya mwisho jana kutinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON, kufuatia ushindi wa dakika za mwisho mwisho. Misri, iliishinda Morocco 1-0 bao lililotiwa wavuni katika dakika ya 87

https://p.dw.com/p/2WfAr
Fußball Afrika-Cup Elfenbeinküste v Togo FBL-AFR-2017-MATCH05-CIV-TOG
Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Misri sasa imejiunga na Ghana ambayo iliishinda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 2-1 katika mpambano mwingine wa jana. Mabao ya Ghana yalifungwa na makaka Jordan Ayew na Andre Ayew. Burkina faso iliibwaga Tunisia kwa kufunga mabao mawili wakati Cameroon iliibandua Senegal kupitia mikwaju ya penalty. Hivyo Misri watashuka dimbani dhidi ya Burkina Faso katika nusu fainali ya kwanza siku ya Jumatano mjini Libreville. Wakati Ghana itakwaruzana na Cameroon mjini Franceville siku ya Alhamisi.

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Yusuf Saumu