1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DIWANIYAH: Marekani yaongoza operesheni dhidi ya wanamgambo

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBW

Ndege za kivita za Marekani nchini Irak,zimeshambulia vituo mbali mbali katika mji wa Diwaniyah ulio kusini mwa mji mkuu Baghdad.Vikosi vya Kiiraki vikisaidiwa na majeshi ya Kimarekani, vimepambana na wanamgambo wa madhehebu ya Kishia kwa siku ya mbili kwa mfululizo.Ripoti zinagongana kuhusu hasara iliyosababishwa na mapigano hayo.Kuambatana na duru ya hospitali moja katika eneo la Diwaniyah,jumla ya maiti 13 na majeruhi 41 walipelekwa kwenye hospitali hiyo katika kipindi cha saa 48.Wakati huo huo,jeshi la Marekani limesema kuwa mapema siku ya Ijumaa, vikosi vilivyoongozwa na Marekani,viliingia mji huo wenye wakaazi wengi wa madhehebu ya Kishia. Kwa mujibu wa jeshi la Marekani,wanamgambo 3 waliuawa na wengine 27 walikamatwa.Operesheni inayoongozwa mjini Diwaniyah inawalenga wanamgambo walio watiifu kwa kiongozi wa kidini mwenye siasa kali,Muqtada al-Sadr.