1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DOHA: OPEC kupunguza uzalishaji wa mafuta

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD18

Mawaziri wa mafuta wa shirika la OPEC,wanaokutana Doha nchini Qatar,wamekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.Shirika la nchi zinazozalisha mafuta ya petroli(OPEC),limetangaza kupunguza mapipa milioni 1.2 kila siku kuanzia tarehe mosi Novemba.Azma ya hatua hiyo ni kuzuia mporomoko wa bei za mafuta,baada ya bei hizo,kati kati ya mwezi wa Julai kufikia kilele.Mawaziri hao wanatambua kuwa kushindwa kwao kuzungumza kwa sauti moja,kulichochea bei za mafuta kuporomoka majuma machache ya nyuma.Kulivuma kuwa mpango wa kupunguza kutoa mapipa milioni moja kila siku, ulipingwa na Saudi Arabia.