1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ikulu ya Marekani:Trump hawezi kuambukiza corona

Sudi Mnette
11 Oktoba 2020

Daktari wa Ikulu ya Marekani, Sean Conley amesemaRais Donald Trump hayupo tena katika kitisho cha kuambukiza virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3jkYm
USA Washington Weißes Haus | Donald Trump, Präsident
Picha: Tom Brenner/Reuters

Taarifa hiyo ya uchunguzi wa kitabibu inatolewa katika kipindi ambacho rais Trump anajiandaa kuanzisha upya mikusanyiko ya kampeni na matukio mengine. Taarifa hiyo ya  daktari huyo inasema Trump ametimiza vigezo vya usalama vya Vituo vya Udhibiti na Kinga kwa hivyo hatazamwi katika hatari ya kueneza maambukizi.

Hakuna taarifa ya Trump kupima virusi tena baada ya kupoma

USA Washington Weißes Haus | Donald Trump, Präsident
Wafuasi wa chama cha RepublicanPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture-alliance

Hata hivyo taarifa hiyo haijasema kama kiongozi huyo kapimwa tena na matokeo ya sasa yaonaonesha kwamba hana hana virusi hivyo. Taarifa hiyo inafuatia pia baada ya hatua ya kiongozi huyo kuonekana kwa mara ya kwanza tangu arejee katika Ikulu ya Marekani, baada ya kubiwa vurusi vya corona. Mamia ya watu walikusanyika jana mchana kwa ajili ya kusikiliza hotuba ya Trump aliyokuwa akiitoa moja kwa moja kutoka katika baraza la Ikulu ya Marekani.

Trump alivua barakao baada ya kujitokeza katika eneo hilo, kwa ajili ya kuhutubia umma huo wa watu, ikiwa ni hatua yake ya mwazo kabisa kuonekana hadharani, katika kipindi ambacho sio zaidi ya wiki tatu Marekani kuingia katika siku ya uchaguzi.

Mashambulizi dhidi ya mgiombea wa chama cha Democratic Joe Biden

Katika siku yake hiyo ya mwanzo Trump hajazungumzia sera yoyote badala yake aliendelea mashambulizi yake ya kawaida kwa mgombea wa chama cha Demockatic Joe Biden, huku akisifia utekelezaji wa sheria kwa umma huo wa watu ambao wengi wao walikuwa wamevaa barakoa na wachache kuzingatia kanuni ya kujitenga.

Trump alikuwa kafungwa bendeji mkononi, mithili ya mtu aliyepata jeraha la kuchomwa sindano, alizungumza kwa dakika 18, ikionekana pungufu ya muda wake wa kawaida. Alionekana mwenye afya. Katika hotuba hiyo aliwashukuru wote waliomtakiwa heri na kumuomba dua apone haraka. Lakini pia pamoja na yeye kuwa mwathirika wa uonjwa huo ambao umegharimu maisha ya Wamarekani 210,00 alidai umeanza kutoweka.

Chanzo: APE