1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DOUALA: Bunge jipya lapigiwa kura Kamerun

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgD

Wapiga kura nchini Kamerun hii leo wanachagua bunge jipya,huku upande wa upinzani ukidai kuwa kuna udanganyifu mkubwa.Ripoti zinasema ,si watu wengi waliojitokeza kupiga kura kwa sababu ni wachache sana walioandikisha majina yao.

Inatazamiwa kuwa uchaguzi wa leo,utaimarisha mamlaka ya Rais Paul Biya anaetawala nchini Kamerun tangu miaka 25 iliopita.Wapinzani, wameshalalamika kuwa upigaji kura umefanyiwa udanganyifu.Wasimamizi wa kimataifa wamesusia uchaguzi huo,baada ya serikali kupuuza wito wa kuunda tume huru ya kusimamia uchaguzi.