1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DOUALA: Juhudi za kusaka na kutambua maiti zaendelea

9 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3p

Tume za waokoaji zinajitahidi kusaka na kutambua wahanga wa ajali ya ndege ya Kenya Airways nchini Cameroon.Ndege hiyo iliangukia eneo la kinamasi muda mfupi baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Douala.Ripoti zinasema kwa sababu mabaki ya ndege yametumbukia eneo lililo chepechepe,hadi sasa maiti 28 zimekusanywa kutoka jumla ya watu 114 waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo. Kisanduku kimoja kinachorekodi data za ndege kimepatikana.Rais Mwai Kibaki wa Kenya ameitangaza Jumatatu ijayo siku ya kuomboleza.