1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DOUALA: Mabaki ya ndege ya Kenya Airways yagunduliwa

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4B

Maafisa wa usafiri wa ndege wa Kenya wamesema, wasaidizi wamegundua mabaki ya ndege ya abiria ya shirika la Kenya Airways iliyopata ajali siku ya Jumamosi kusini mwa Cameroon.Wamesema,mabaki ya ndege hiyo yameonekana katika eneo la kinamasi kama kilomita 20 kusini-mashariki ya uwanja wa ndege wa Cameroon,Douala.Kwa hivi sasa,hakuna habari ikiwa kuna watu walionusurika.Safari ya ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ilianzia mji mkuu wa Ivory Coast,Abidjan na ilitua Douala nchini Cameroon ikiwa njiani kurejea mji mkuu wa Kenya,Nairobi.Ndege hiyo iliyokuwa takriban mpya, ilipotea muda mfupi tu baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Douala ikiwa na watu 114.Wakati huo mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika eneo hilo.

KABUL:

Mwanajeshi wa Kiafghanistan amewapiga risasi na kuwaua wanajeshi 2 wa Kimarekani mbele ya jela inayolindwa vikali karibu na mji mkuu Kabul. Wamarekani wengine 2 pia walijeruhiwa.Sababu ya shambulio la mwanajeshi huyo wa Afghanistan haijulikani.Msemaji wa kijeshi amearifu kuwa kufuatia shambulio hilo,mwanajeshi huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na wenzake.