1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Polisi yamzuia Fayulu kuhutubia wafuasi wake

Daniel Gakuba
21 Januari 2019

Polisi wamezuia wafuasi wa Martin Fayulu kukusanyika kwenye makao makuu ya chama chake alitakorajiwa kuwahutubia. Ingawa Korti ya Katiba imethibitisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu anadai ameibiwa ushindi wake.

https://p.dw.com/p/3BukS
DR Kongo Unterstützer von Martin Fayulu in Kinshasa
Picha: Reuters/K. Katombe

 

Msemaji wa Martin Fayulu Eve Bazaiba amesema polisi walivamia mahali ambako Fayulu alikusudia kuwahutubia wafuasi wake, na kulibeba jukwaa na vipazasauti vilivyokuwa vimeandaliwa.

''Wamevikamata vyombo vyote na kuwakamata pia watu, na sijui wamewapeleka wapi.'' amelalamika Bazaiba na kuongeza, ''nilipouliza kinachoendelea, nimeambiwa polisi wanacho kibali cha kuwazuia watu kuingia na kutoka.''

Licha ya kutawanywa na polisi baadhi ya wafuasi wa vuguvugu la upinzani la LAMUKA linalomuunga mkono Fayulu waliendelea kusubiri kuwasili kwa kiongozi wao kwenye makao makuu ya chama cha MLC.

Fayulu na wafuasi wake ambao wamepinga matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi na kujitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi huo amesema kwamba ni lazima raia wa kongo wapewe haki zao. 

DR Kongo Martin Fayulu in Kinshasa
Martin Fayulu anayedai kuwa amepokonywa ushindiPicha: Reuters/B. Ratner

''Tunachotaka ni kupata haki kulingana na matokeo ya uchaguzi, kwa sababu tuna uhakika kwamba tulishinda,'' amesema msemaji wa Fayulu Eve Bazaiba, na alipoulizwa watafanya nini kuhakikisha wanafanikiwa, amesema watazidi kukazana kwa sababu 'sheria iko upande wetu.''

Kuapishwa kwa Tshisekedi kwasogezwa nyuma

Wakati huohuo, mandalizi kwa ajili ya kuapishwa kwa rais mteule Felix Tshisekedi yanaendelea mjini Kinshasa. Sherehe hiyo iliotarajiwa kufanyika Jumannen imeahirishwa hadi Alhamisi, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Lambert Mende msemaji wa serikali inayoondoka madarakani.

Mahali patakapofanyika sherehe hiyo bado kufahamika, lakini wafuasi wa chama cha UDPS cha Tshisekedi waliomba kiongozi wao aapishwe kwenye uwanja wa kandanda wa Kinshasa ilikuwaruhusu washiriki pia.

Ni kwa mara a kwanza Kongo itashuhudia kuapishwa kwa rais mpya kufuatia kuchukuwa madaraka kwa njia ya amani kutoka kwa rais mwingine.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo,DW Kinshasa.

Mhariri: Iddi Ssessanga