1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Drogba aondoka Chelsea kwa mara ya pili

25 Mei 2015

Mshambuliaji wa Chelsea raia wa Cote d'Ivoire Didier Drogba anaihama klabu hiyo kwa mara ya pili.

https://p.dw.com/p/1FWBh
Didier Drogba
Picha: imago/Panoramic

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa na klabu hiyo mwaka 2004 na amefunga mabao 164 katika mechi 381.

Akizugnumza kabla ya mechi ya mwisho ya msimu ambayo pia ilikuwa yake ya mwisho kama mchezaji wa Chelsea, dhidi ya Sunderland uwanjani Stamford Bridge, Didier aliiambia tovuti ya Chelsea kuwa angependa kucheza tena kwa msimu mmoja zaidi na kwa hilo kufanikiwa itabidi ahamie kilabu nyengine. Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho alimsajili kwa mara ya pili Drogba kwa kandarasi ya mwaka mmoja baada ya kuondoka Galatasaray ya Uturuki.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu