1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muda unayoyoma kuokoa mimea na wanyama wa dunia

Yusra Buwayhid
24 Machi 2018

Ripoti tano mpya zilizozinduliwa katika mkutano mkuu wa viumbe hai wa Umoja wa Mataifa Colombia zinatahadharisha juu ya hali mbaya ya viumbe hai duniani. Lakini pia zinashauri juu ya namna ya kupambana na hali hiyo.

https://p.dw.com/p/2utrp
Ecuador Amazonas Regenwald
Picha: picture-alliance/robertharding

Wajumbe katika mkutano mkuu wa kimataifa juu ya viumbe hai huko Medellín, Colombia wameshtuka baada ya kutolewa ushahidi mpya juu ya hali ya viumbe hai duniani.

Wajumbe 750 kutoka nchi 115 wanakutana katika kikao cha sita cha Jukwaa la Kisayansi na Sera Baina ya Serikali juu ya Viumbe Hai na Mfumo wa Ekolojia ambao mara nyingi hujulikana kama "IPCC kwa ajili ya viumbe hai."

Jukwaa hilo lilipewa kazi na Umoja wa Mataifa mwaka 2012 kutoa ushahidi bora zaidi ili kuweze kufanywa maamuzi bora ya sera juu ya jinsi ya kulinda mazingira katika wakati ambapo dunia inaendelea kukabiliwa na shinikizo kubwa kabisa.

Infografik The great acceleration Englisch
Mahitaji ya rasilimali ya binaadamu yameongezeka kwa kiasi kikubwa katika muda mfupi

Ripoti hizo tano, ambazo zilitayarishwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na wataalamu wa kimataifa wapatao 550, zinatoa tathmini ya kikanda juu ya viumbe hai barani Afrika, Amerika Kaskazini na Amerika Kusini, Asia Pasifiki, Ulaya na Asia ya Kati. Ripoti ya tano inatoa tathmini juu ya hali ya uharibifu wa ardhi duniani kote.

Ripoti hizo zinahitimisha kwamba kwa upande wa Amerika, spishi zimepungua kwa asilimia 31 ikilinganishwa na wakati walipowasili walowezi kutoka barani Ulaya. Athari za mabadiliko ya tabia nchi zikiwa zinaongezeka zimechangia sababu nyingine, kupotea huko kwa spishi kunatabiriwa kufika asilimia 40 ifikapo 2050.

Katika Afrika, kilomita 500,000 za mraba za ardhi tayari zinakadiriwa kuwa zimeharibiwa na matumizi makubwa ya rasilimali za asili, mmomonyoko wa ardhi, myeyusho wa chumvi na uchafuzi wa mazingira. Katika Umoja wa Ulaya, ni 7% pekee ya spishi za baharini na 9% ya aina za viumbe vinavyoishi baharini zinazoonyesha "hali nzuri ya hifadhi". 66% ya aina za viumbe vinavyoishi baharini inaonyesha "hali mbaya ya hifadhi", na aina nyingine zimeorodheshwa kama "haijulikani".

Indonesien Artenvielfalt am Riff
Viumbe wa bahariniPicha: picture-alliance/blickwinkel

Kanda ya Asia-Pasifiki imeonyesha matokeo ya kutia moyo zaidi. Katika miaka 25 iliyopita, maeneo ya bahari yanayohifadhiwa katika kanda hiyo yameongezeka kwa takriban 14% na maeneo ya ardhini yanayohifadhiwa yameongezeka kwa 0.3%. Maeneo ya misitu yameongezeka kwa asilimia 2.5%.

Ripoti hizo pia zimegundua ukosefu wa maendeleo katika mipango mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kuhusu viumbe hai, ikiwa ni pamoja na Mpango wa Mikakati wa Viumbe Hai 2011-2020 na malengo yanayohusu viumbe hai, yaliyofikiwa na makundi tofauti yaliyohusika katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Viumbe Hai uliofikiwa katika mkutano wao huko Aichi, Japan mwaka 2010.

Hatua za kumbambana na tatizo

Lakini pamoja na kuonyesha hali ya kutisha, ripoti hizo pia zimetoa matumaini mapya ya kupambana na tatizo hilo. Mapendekezo maalum kuhusu jinsi watunga sera wanavyoweza kusitisha au kurekebisha uharibifu wa viumbe hai katika maeneo tofauti.

"Zikiwekwa pamoja, ripoti hizi tano za ukaguzi zinawakilisha mchango mmoja muhimu wa kitaalamu kwa ufahamu wetu wa kimataifa wa viumbe hai na mfumo wa ekolojia wa miaka kumi iliyopita," alisema Robert Watson, mwenyekiti wa mkutano huo. "Tathmini hizi zitatoa ufahamu ambao haukuwahi kushuhudiwa juu ya hali ya viumbe hai duniani na ubora wa ardhi, vitu viwili ambavyo ni muhimu kwa ubora wa maisha na afya, na mifumo ya ekolojia."

Infografik Decline in vertebrate populations, englisch
Idadi ya wanyama na miti imepungua na ya binadamu imeongezeka

Uhitaji wa hatua haujawahi kuwa muhimu zaidi kuliko wakati huu tulionao. Kati ya 1970 na 2012, uti wa mgongo wa hisa za kila mwaka zilipungua kwa zaidi ya nusu duniani kote. Kupungua huko kwa sasa ni asilimia mbili kwa mwaka. Wakati huo huo, kila mwaka binadamu hutumia rasilimali nyingi zaidi kuliko uwezo wa dunia. Matokeo yake ni kwamba tunaharibu mifumo muhimu ya ekolojia.

Madhara ya mabadiliko ya tabia nchi yatasababisha tatizo kuwa baya zaidi, isipokuwa pale wasimamizi watakapochukua hatua. Lakini Anne Larigauderie, katibu mtendaji wa IPBES, anaamini ushahidi mpya uliotolewa utahamasisha kuchukuliwa hatua.


"Kuna ufahamu mkubwa wa haja ya mazingira kujumuishwa katika mipango yote ya maendeleo, na IPBES inajivunia kuwapa wafanya maamuzi ulimwenguni kote ushahidi wanaouhitaji kutunga sera bora na kuchukua hatua bora zaidi kuweza kuwa na maisha ya baadae yaliyo enedelevu tunayoyataka" amesema.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/DW

Mhariri: Sylvia Mwehozi