1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya pili ya Kombe la afrika la klabu bingwa.

13 Machi 2009

Beckenbauer adai Hoffenheim kutwaa ubingwa wa Bundesliga .

https://p.dw.com/p/HBTh
Franz BeckenbauerPicha: DW / Arnulf Boettcher

Rais wa mabingwa wa Ujerumani-Bayern Munich,Franz Beckenbauer asema Hoffenheim,tuimu iliopanda daraja ya kwanza msimu huu tu, yaweza kutoroka na taji la ubingwa wa Bundesliga-

Mastadi wa TP Mazembe, wanarudi nyumbani mwishoni wiki hii kwa Kombe la klabu bingwa baada ya kuitawaza timu ya taifa ya D.R.C mwishoni mwa wiki iliopita mabingwa wa kombe la Afrika huko Abidjan kwa kuitimua Ghana 2-0.

Duru ya pili ya Kombe la Afrika lła klabu bingwa inaanza.

Harambee Stars-Kenya na timu yake ya rugby zajiandaa kwa Kombe la dunia.

Kinyanganyiro cha kombe la klabu bingwa barani Afrika kinarudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii na macho yanakodolewa mbali na mabingwa CS Sfaxien ya Tunisia inayoikaribisha nyumbani Al Ahly -Benghazi ya Libya ,bali mastadi wa TP Mazembe waliochangia ushindi wa Simba wa jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo jumapili iliopżita waliponguruma mbele ya Ghana na kurudi Kinshasa na Kombe.

TP Mazembe ilioundwa miaka 70 iliopita mjini Lumbubashi, inaikaribisha Petro Atletico ya Angola katika duru ya pili ya kombe la klabu bingwa.

TP mazembe ilichangia wachezaji 14 katika kikosi cha timu ya Taifa kilichotamba Abidjan wiki iliopita.Isitoshe, kocha wa timu ya Taifa Mutumbile "Obama" Santos pia ni kocha wa Mazembe-klabu ambayo 1968, iliiandika historia kuwa ya kwanza kutwaa ubingwa wa kombe la Afrika mara 2 mfululizo.2002,TP Mazembe alikaribia kulitwaa tena lakini, ilitimuliwa nje ya nusu-finali na Zamallek ya Misri.

Mabi Mputu -mshambulizi wa Kongo alietamba huko Ivory Coast na kutia moja kati ya mabao 7 ya Kongo huko atabidi kuogopwa na waangola Petro Atletico.Petro ikiongozwa na kocha wao mreno Bernardino Pedroto ilishinda kwa urahisi mpambano wake wa nyumbani na ugenini duru iliopita ilipocheza na Royal Leopards ya Swaziland mwezi uliopita na wanakuja Lumbubashi wakiwa wametamba mara tatu mfululizo katika Ligi ya Angola.

Mabingwa mara kadhaa Al Ahly ya Misri, waliotwaa Kombe hili jumla ya mara 6 na rekodi ni miongoni mwa timu 11 zilzobidi kutocheza duru ya kwanza na wanaanza kutamba leo nyumbani mbele ya mabingwa wa tanzania Young Africans.Kipa wa Al Ahly mpalestina Ramzi saleh amechukua nafasi ya Abdulhamid,langoni-kipa wa mabingwa mwaka jana .Lakini itabidi achunge vishindo vya wsashambulizi 2 wa Younga Boniface Ambani na Mrisho Ngasa,kwani kwa pamopja waliionea Etoile d-Or Mirontsy ya visiwa vya Comoro kwa mabao 14-1 kufuatia duru mbili.Mchicha kama huo hawataupata lakini mbele ya Al Ahly.

Al Ahly na TP Mazembe ni miongoni mwa mabingwa 9 wa Kombe hili walio uwanjani mwishoni mwa wiki hii .Mabingwa mara 3 Canon Yaounde ya Kamerun, wanacheza Angola ikitimiza huko miadi yake na Primeiro Agosto.Washindi wa kombe la washindi barani Afrika 1991, Club Africain ya Tunisia wanaikaribisha nyumbani Djoliba ya Mali.

Etoile du saheil waliowasangaza Al Ahgly,na kuwapokonya taji 2007,wameimarisha kikosi chao kwa kuwaajiri wachezaji wapya kutoka Nigeria,Brazil na Columbia kujiweka tayari kwa zahama ya nyumbani na ASO Chlef ya Algeria.

ASEC Mimosas ya Ivory Coast,Kabylie ya Algeria na Asante kotoko ya Ghana zinakumbana kila moja na Etoile Filante ya B.Faso,Al-Ahly ya Libya na Al-ittihad ya Morocco.FAR rabat inabuburushana uwanjani na Heartland ya Nigeria.

Tugeukie sasa Bundesliga na Ligi mashuhuri barani Ulaya:

Baada ya timu za Ujerumani kukata tiketi za duru ijayo-za vikombe vya Ulaya -champions League kwa mabingwa B.Munich na UEFA kwa Bremen na pengine Hamburg, Bundesliga imerudi uwanjani. Viongozi wa ligi Hertha Berlin wanacheza leo na Bayer Leverkusen,timu ya zamani ya mshambulizi wao Andrey Voronin.Hoffenheim inapambana na Frankfurt wakati FC cologne iko nyumbani ikiikaribisha B.Moenchengladbach.Bochum inaahidi kuitoa jasho mabingwa Bayern Munich.

Rais wa Bayern Munich Franz Beckenbauer na nahodha na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani aliagua wiki hii kwamba, kwa maoni yake Hoffenheim,klabu iliopanda msimu huu tu daraja ya kwanza kutoka ya pili, ndio mwishoe itatwaa ubingwa.Hii itakua mara ya pili tangu 1999 pale Kaiserslauten ilipofanya maajabu kama hayo.

Beckenbauer, ameliambia gazeti la BILD jana kuwa Hoffenheim ndio timu pekee inayotimiza masgharti yote ya timu yenye ufanisi.Akaisifu kwamba Hoffenheim ina uwezo wa kugeuza mchezo haraka kabisa na ina wachezaji ambao wakati wote wako mbioni na haoni udhaifu wowote katika timu hii chipukizi iliozusha msangao mkubwa msimu huu. Hoffenheim kabla changamoto za jioni hii iko nafasi ya pili nyuma ya Hertha Berlin pamoja na Bayern Munich.Lakini wako pointi 4 nyuma ya viongozi Berlin.