m-dw.de - Anwani yetu ni rahisi kuikumbuka na kuitumia. Soma taarifa za DW za kimataifa na uchambuzi zilizotayarishwa kwa ajili yako ukiwa kwenye mwendo.
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za kundi la G7 wamezungumzia wasiwasi wao kuhusu makampuni ya China kupeleka vifaa vya kijeshi na vipuri vya silaha nchini Urusi kwa ajili ya kulisaidia jeshi la nchi hiyo.
Mwandishi mmoja wa habari nchini Burundi ameshtakiwa kwa kosa la kuhatarisha usalama wa ndani, ambalo linamuweka katika hatari ya kukabiliwa na kifungo cha maisha jela.
Duru zinasema Israel imefanya shambulio katika ardhi ya Iran mapema leo Ijumaa, siku kadhaa baada ya Iran kuishambulia kwa makombora na droni nchi hiyo katika hatua ya kulipiza kisasi. Hatua hiyo imezidisha wasiwasi wa kutanuka kwa mzozo katika kanda ya Mashariki ya Kati. #kurunzi