1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

El-Sisi kuwa mwenyekiti wa AU

Sekione Kitojo
10 Februari 2019

Karibu  miaka  sita  baada  ya  Umoja  wa  Afrika  kuiweka  kando, Misri itachukua  uongozi wa  Umoja  huo na  kuimarisha  madaraka yake inatarajiwa  kuwa  ajenda  ya  nchi  hiyo.

https://p.dw.com/p/3D4ZG
Ägypten Präsident Abdel Fattah Al-Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah el-SisiPicha: picture -alliance/Sputnik/Vitaliy Belousov

Kipindi cha  Misri cha  uongozi "huenda  kikaelekezwa  katika usalama  na  ulinzi wa  amani", amesema  Ashraf Swelam, ambae anaongoza  taasisi  ya  uchunguzi wa  masuala  ya  kisiasa  yenye uhusiano  na  wizara  ya  mambo  ya  kigeni  ya  nchi  hiyo.

Mwenyekiti wa  AU  anayeingia  madarakani   rais Abdel Fattah al-Sisi anaonekana  kuelekea  kutolenga "mageuzi  ya  masuala  ya fedha  na  utawala" kama  ilivyokuwa  kwa  mtangulizi wake , Swelam aliongeza.

Äthiopien AU-Gipfel in Addis Adeba
Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Afrika Paul Kagame wa RwandaPicha: Getty Images/AFP/M. Bhuiyan

Mageuzi  ya  aina  hiyo  yalikuwa alama muhimu  ya  mwenyekiti   wa AU  anayeondoka  madarakani Paul Kagame . Rais  huyo  wa Rwanda  amekuwa  akisukuma  kuundwa   kwa  mfuko  wa kodi  ya mauzo  ya  biadhaa  zinazoingizwa  katika  bara  hilo  kutoka  nje   na kupunguza  utegemezi  wa  bara  hilo kwa wafadhili  wa  nje, ambao bado  wanalipa  fedha  kwa  ajili ya  nusu  ya  bajeti ya  taasisi  hiyo kila  mwaka.

Mataifa  makubwa  ya  Afrika

Mwanadiplomasia  wa  Afrika  aliliambia  shirika  la  habari  la  AFP kwamba  Misri , pamoja  na  mataifa  mengine  yenye uchumi mkubwa  Afrika  kusini  na  Nigeria  hazitaki AU  yenye  nguvu.

Mwanadiplomasia  huyo, ambaye  amekuwa  akifuatilia  masuala  ya AU kwa  muda  wa  muongo  mmoja, amesema  Misri  "Haijasahau" kusitishwa  kwake  uanachama  mwaka  2013.

Ägypten Afrika-Treffen COMESA, EAC und SADC
Rais el-Sisi akiwa pamoja na viongozi wa mataifa ya Afrika mjini Sharm el-Sheikh nchini MisriPicha: Imago/Xinhua

Kuwekwa  kando  kwa  karibu  mwaka  kutoka  katika  Umoja  wa Afrika  kulikuja  baada  ya  jeshi  la  Misri  kumuondoa  madarakani rais Mohamed Mursi, ambaye  mwaka  2012  alikuwa  rais  wa kwanza  nchini  humo  aliyechaguliwa  kidemokrasia.

Sisi  anatarajiwea  kuchukua  hatamu za  kuuongoza Umoja  wa Afrika  katika  baraza  la  mataifa  hayo  la  miaka  miwili, ambalo lianza kikao  chake  Februari  10  na  11  katika  makao  makuu  ya Umoja  huo  katika  mji  mkuu  wa  Ethiopia, Addis Ababa.

Kama  kawaida, mizozo kadhaa  ya  bara  hiyo  ya  kiusalama itakuwa juu  katika  ajenda ya  viongozi  hao. Pendekezo  la  Rwanda la  kupata  mfuko  wa  kugharamia bajeti  ya  bara hilo  pia  itakuwa sehemu  ya  majadiliano.

Lakini pendekezo  hilo  limekumbana  na  upinzani  sio  tu  kutoka Misri, lakini  mataifa  mengi  wanachama, kwa  hiyo  inawezekana kuwa  halitapita.

Deutschland Ägyptischer Präsident Al-Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah el-SisiPicha: Getty Images/A. Berry

Mageuzi katika  AU

Mageuzi  ya  halmashauri  ya  AU ni  mada  nyingine  nyeti  zaidi. Novemba  mwaka  2018, mataifa  mengi  yalikataa  pendekezo  la kutoa  kwa  chombo  hicho  cha  utendaji  cha  AU, madaraka  ya kuwateua wabunge  pamoja  na   makamishina.

Lakini Misri  "wako tayari" katika  kusukuma  mageuzi  mengine  ya AU, kwa  mujibu wa  afisa  mmoja  wa  Umoja  huo.

Somalia Landminen
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia kutoka UgandaPicha: Getty Images/AFP/A. Abikar

Juhudi moja  muhimu inayoungwa  mkono  na  Cairo ni eneo  la biashara  huru  la  bara  hilo  CFTA, juhudi zilizokubalika  na  mataifa 44  kati  ya  55  wanachama mwezi  Machi 2018.

Soko  la  pamoja  ni nguzo  ya  mpango  wa  Umoja  wa  Afrika wa "Ajenda 2063", uliotayarishwa  kama  mfumo  wa  mkakati  kwa  ajili ya  mabadiliko  ya  uchumi  wa  jamii.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Grace Patricia Kabogo