1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Elbaradei yuko Iran kwa mazungumzo ya Nuklia

11 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Co0o

TEHRAN

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Nuklia IAEA Mohammed Elbaradei amewasili mjini Tehran hii leo tayari kwa mazungumzo ya kujadili juu ya maswala kadhaa yaliyosalia katika mgogoro wa Nuklia wa Iran.

Elbaradei anajaribu kuitia msukumo Iran kuweka wazi mipango yake yote ya Kinuklia.Mkuu huyo wa shirika la IAEA anakutana leo hii na maafisa wa ngazi ya juu wa Iran akiwemo rais Mahmoud Ahmednejad.Iran imekuwa ikishikilia msimamo wake kwamba juhudi zake za kurutubisha madini ya Uranium ni kwa ajili ya matumizi ya kiraia na wala sio kijeshi.Hata hivyo mataifa mengi ya magharibi yanahofia kwamba nchi hiyo inaweza ikatengeneza mabomu ya Nuklia kupitia mpango wake huo,hofu ambayo imesisitizwa wiki hii na rais George Bush akisema Iran ni tishio kwa amani ya dunia.