1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Elimu barani Afrika

24 Machi 2010

Zaidi ya walimu milioni moja wanahitajika barani Afrika.

https://p.dw.com/p/MbD5
Wanafunzi wa shule za Afrika wakiwa katika masomo ya kompyuta.Picha: picture-alliance/dpa

Kuna haja ya kuwaajiri walimu milioni moja  na laki kumi na nne katika bara la Afrika iwapo tuna azma ya kutimiza lengo la pili katika malengo ya milenia. Haja hii inatoa changamoto nyingi kwa serikali mbalimbali barani Afrika kwa sababu sio tu kutoa elimu bali pia iwe ni ya kiwango cha juu.

Kutokana na haya nchi za kiafrika zinalazimika  kuwafunza walimu kote barani Afrika , mfumo wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa viwango mbalimbali ambapo mfumo huu unahusu mwalimu kuwa na jukumu la kuwafunza  wanafunzi wenye umri tofauti  katika darasa moja, na utawezekana kukiwepo makadirio mema ya fedha za utumizi kwenye idara ya elimu pamoja na kutengenezwa kwa mtaala  na mafunzo kutolewa kwa walimu wenyewe.

Mfumo huu vilevile  huenda ukatoa suluhu kwa elimu ya kiwango cha juu kwa sababu inatoa  fursa kwa kuendeleza shule nyingi katika maeneo ya mashinani ambayo ina maana ni wanafunzi wengi watakaoweza kupata elimu kukiwa na  idadi ndogo ya waalimu

Katika nchi nyingi barani Afrika mfumo huu wa elimu unatumika kutokana na hali duni za kiuchumi na hali za maisha ya watu.

Virgilio Huvanne ambaye ni mshirikishi katika shirika la maendeleo kwa elimu barani Afrika ADEA anasema kwamba ni matumaini kwamba mfumo huu wa elimu utaweza kutumika katika nchi nyingi Afrika hususan katika nchi kama vile  Zambia, Uganda,  Lesotho na Namibia ambapo utawarahisishia wanafunzi wanoishi maeneo yaa mashinani msimokuwa na shule na kawaida wanafunzi hulazimika kusafiri mpaka miji aina moja tu unaotolewa.

Hatahivyo Huvanne anasema kwamba  kuna pengo katika sera sababu ni kwamba serikali za nchi nyingi  bado hazijajuwa manufaa ya mfumo huu na kwamba wengi huutazama  kama wa kiwango cha chini na unaotumika kwa muda hadi pale mafunzo ya kawaida yatakopoweza kutolewa.

Afisaa mkuu wa shirika la ADEA ambalo ni shirika la kuendeleza elimu barani Afrika, Colbert  De Arboleda anaeleza kwamba nchini Columbia kama ilivyo Afrika elimu inatolewa lakini swala ni ubora wa elimu hiyo ambapo ni duni sana  na kupelekea kwa wanafunzi wengi kutoroka shuleni,lakini hali hii ilibadilika pale serikali ya nchi hiyo ilipoidhinisha mpango kwa kubadilisha mfumoili kumkidhi  mwanafunzi.

Mfano huu Colbert anasema unadhihirisha jinsi inavyowezekana kundeleza ubora wa elimu hata  kukiwepo uhaba wa fedha na anaongeza kwamba shule zinazofunza mfumo huu hufanya vizuri zaidi kushinda zile za kawaida.

Kutokana na haya afisa wa elimu katika taasisi ya kuendeleza elimu nchini Namibia anasema kwamba kuna haja ya  kuubadilisha mfumo wa elimu ili kumnufaisha mwanafunzi kinyume na  hali ilivyo hivi sasa.

Mwandishi: Maryam Dodo Abdalla/IPS

Mhariri:Abdul-Rahman