1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kujihusisha – Elimu ya Siasa na kujishirikisha

7 Januari 2010

Ushiriki kila mara ni rahisi. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinawaongoza wasikilizaji kupita katika ulimwengu wa siasa ili kuwaonyesha nini maana ya kuwa mwanaharakati.

https://p.dw.com/p/Dn9u
Picha: gettyimages

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“inaungana na vijana watatu ambao wana ndoto ya kufungua shule ya muzuki. Upatikanaji wa vibali muhimu pamoja na fedha za kutosha vinajitokeza kuwa ni vikwazo. Wanajifunza jinsi ya kuungana na wanasiasa wa maeneo yao, asasi zisizokuwa za kiserikali pamoja na taasisi za jamii ili kuweza kufanikisha ndoto yao.

Kuibadilisha dunia kuptia elimu

Kupitia mchezo huu wa radio , „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ inatoa mwanga juu ya harakati kadhaa za kisiasa na kijamii ambazo zinajenga hali ya maisha hii leo. Inawapa wasilikizaji mtazamo juu ya nani anaamua nini katika maisha yanayowazunguka, na kuwawezesha kutambua vipi wanaweza kushiriki katika maamuzi na kuweza sauti zao kusikika. Lakini haya si masomo ya kisiasa ambayo hayana maana, „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ pia kinajumuisha burudani ya muziki ili kuyafanya masomo haya ya kufurahisha.

„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“kinapatikana katika lugha sita: Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama ukitaka kusikiliza vipindi hivi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.dw-world.de/lbe. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ inadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.