1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ELTVILLE: Mkutano unajadili changamoto za Afrika

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AB

Rais Horst Köhler wa Ujerumani anaetoa kipaumbele kupiga vita umasikini barani Afrika amefungua mkutano kuhusu Bara la Afrika katika mji wa Eltville nchini Ujerumani.Miongoni mwa mada zinazojadiliwa katika mkutano huo ni changamoto za utandawazi,uhamiaji kutoka Afrika na athari zake kwa nchi zinazofuatwa kama vile barani Ulaya.

Rais Köhler amesema,anaamini kuwa utandawazi utaweza kutekelezwa kwa manufaa ya kila mmoja ikiwa tu kutakuwepo ushirikiano ulio na haki sawa.

Mkutano huo unahudhuriwa na marais wa Msumbiji, Botswana,Madagaskar,Benin na Nigeria na vile vile wajumbe wa sekta za kisiasa na kiuchumi.

Huu ni mkutano wa tatu kusimamiwa na Rais Köhler ambae hapo zamani alikuwa mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF mjini Washington.Mkutano wa kwanza ulifanywa Novemba mwaka 2005 karibu na mji wa Bonn nchini Ujerumani na wa pili ulikuwa Januari mwaka 2007 katika mji wa Accra nchini Ghana.