1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

England na Scotland huenda zikaadhibiwa na FIFA

Sekione Kitojo
12 Novemba 2016

England na Scotland zinalazimika kusubiri na kuona iwapo zitakabiliwa na vikwazo vya FIFA baada ya timu za taifa za nchi hizo kufanya kumbukumbu ya watu waliofariki katika vita vikuu vya kwanza vya dunia mwaka.

https://p.dw.com/p/2SaoL
Fußball WM-Qualifikation England gegen Schottland
Katika mchezo kati ya England na Scotland wachezaji walivaa ua na kitambaa cheusi mkononiPicha: Picture-Alliance/dpa/G. Penny

England  na  Scotland  zinakabiliwa  na  hali  ya  sintofahamu  ya kusubiri  kuona  iwapo zitakabiliwa  na  vikwazo  baada  ya kuchukua  hatua  ya  kufanya  kumbukumbu  ya  maombolezi  kwa watu  waliofariki  katika  vita  nchini  Uingereza  katika  mchezo  wao wa  kufuzu  kucheza  katika  kombe  la  dunia.

Timu  hizo  mbili, zikiongozwa  na  nahodha  wa  timu  ya  taifa  ya England , Wayne  Rooney  na  mwenzake  wa  Scotland  Darren Fletcher , walivaa  kitambaa  cheusi  mkononi  pamoja  na  ua jekundu  katika  mchezo  wao  jana  Ijumaa  uwanjani  Wembley, ambapo  wenyeji  walishinda  kwa  mabao 3-0.

Fußball WM-Qualifikation England gegen Schottland
Pambano katio ya England na Scotland, ambapo , England iliishinda Scotland mabao 3-0Picha: picture alliance/AA/T. Akmen

Shirikisho  la  kandanda  duniani  FIFA  limeonya  hatua  hiyo  kuwa inaweza  kukiuka  sheria  inayopiga  marufuku "kauli mbiu za  kisiasa, kidini  ama za  binafsi, taarifa , ama  picha".

Akizungumza   kabla  ya  mchezo  huo , kocha  wa  mpito  wa England  Gareth Southgate  alisema: "Tunafuraha kwamba  tunaweza kuwaenzi watu  waliojitoa  muhanga  kuitetea  nchi  yetu  ambao wametangulia."

Watu  nchini  Uingereza  kwa kawaida  huvaa  alama  ya  maua katika  siku  zinazoelekea  Novemba  11, siku  ya  Armistice ilipotiwa saini  mwishoni  mwa  vita  vikuu  vya  kwanza  vya  dunia  mwaka 1918, kuwakumbuka  watu  waliofariki  nchini  humo  kutokana  na vita  hivyo.Vyama  vya  kandanda  vya England  na  Scotland vinaweza  kuadhibiwa  kwa  hatua  za  kinidhamu  iwapo  kamisaa wa  mchezo   huo  kutoka  FIFA  atataja  kuhusu  vitambaa  hivyo vya  mkononi  katika  ripoti  yake  kuhusu  mchezo  huo.

 

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Sylvia  Mwehozi