1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eritrea, Ethiopia zachukua hatua kujongeleana

Iddi Ssessanga
20 Juni 2018

Rais Wa Eritrea Isaias Afwerk amevunja ukimya wa wiki kadhaa na kuitikia hatua za maridhiano kutoka kwa hasimu wake mkuu Ethiopia, na kuibua matumaini ya mwanzo mpya katika eneo hilo la pembe ya Afrika.

https://p.dw.com/p/2zxCn
Eritrea Präsident Isaias Afwerki
Picha: Eritrea Minister of Information/Y.G. Meskel

Huo ndiyo ulikuwa mwitikio wa kwanza kutoka Eritrea, moja ya mataifa yanaongozwa kwa usiri mkubwa na mkono wa chuma barani Afrika, kwa ahadi ya Abiy alioitoa mwezi huu kuheshimu masharti yote ya makubaliano ya amani yaliohitmisha vita vya mwaka 1998 hadi 2000 kati ya majirani hao wa pembe ya Afrika.

Mkuu wa shughuli za ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia alisema waziri mkuu Abiy amekaribisha taarifa ya Isaias na kuahidi kwamba ujumbe wa Eritrea utakaribishwa vizuri na kwa njia njema.

Vita kati ya mataifa hayo vililinganishwa na vita kuu vya kwanza vya Dunia, ambapo mawimbi ya wanajeshi waliolaazimishwa kupitia maeneo yaliotegwa mabomu ya ardhini kwenda Eritrea, waliuawa kwa kumiminiwa risasi. Jumla ya wanajeshi wapatao elfu 80 wanaaminika waliuawa katika vita hivyo.

Addis Abeba, Äthiopien, Äthiopischer Premierminister Abiy Ahmed im Parlament
Waziri mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy.Picha: DW/Y.Geberegziabher

Migogoro juu ya mpaka wenye shughuli nyingi za kijeshi kati ya mataifa hayo, na hasa mji wa Badme, imeendelea kuzigombanisha pande hizo, huku Asmara ikitumia kisingizio cha kitisho kutoka Ethiopia kuhalalisha matumizi makubwa ya kijeshi na utumishi wa laazima jeshini.

Hata hivyo, Abiy mwenye umri wa miaka 41 na mwanajeshi wa zamani ambaye ameainisha mkururo wa mabadiliko kadhaa makubwa tangu alipochukuwa madaraka mwezi Machi, aliwashangaza wa Ethiopia mwezi huu kwa kusema alikuwa tayari kuheshimu maamuzi ya kimataifa ambayo yanauweka mji wa Badme, ambao Ethiopia ilikataa kuuachia, nchini Eritrea.

Shauku ya amani ya muda mrefu

Isaias amesema muafaka huo, ambao unauwezekano mkubwa wa kukabiliwa na upinzani kutoka wanasiasa wenye msimamo mkali kutoka chama tawala cha EPRDF, umetokana na shauku ya mataifa yote mawili kufikia amani ya muda mrefu.

"Kama ilivyo kwa Eritrea, watu wa Ethiopia wanataka kuishi kwa amani na jirani yao.Ishara chanya zilizotolewa katika siku hizi chache zilizopita zinaweza kuonekana kama kielelezo cha chaguo hilo la wengi," alisema rais huyo katika siku ya mashahidi mjini Asmara siku ya Jumatano.

Karte Infografik Umstrittene Gebiete Äthiopien Eritrea DEU
Ramani inayoonyesha mji wa Badme ambao umekuwa chimbuko la mzozo kati ya Ethiopia na Eritrea.

"Kwa sababu hii, na nje ya mtazamo finyu wa kutaka kujipigia debe na kutumia fursa, tutatuma ujumbe kwenda Addis Ababa kupima maendeleo ya sasa moja kwa moja kwa kina na pia kujadili hatua endelevu za baadae."

Taifa la bahari ya Sham la Eritrea liliwahi kuwa sehemu ya Ethiopia na lilikuwa linajumlisha pwani yake yote hadi mwaka 1993 lilipopiga kura kujitenga na jirani yake huyo wa kusini, na kuifanya Ethiopia kuwa taifa lisilo na njia ya bahari.

Mwaka 1998, tofauti kuhusu michoro ya mpaka wao wa pamoja ilisababisha vita vilivyogharimu kaisah ya watu karibu lefu 80. Tume ya mipaka ilioungwa mkono na umoja wa Mataifa ililigawanya eneo linalozozaniwa mwaka 2002 kati ya mataifa hayo, lakini Ethiopia likataa uamuzi huo.

Mwandishi: Iddi ssessanga/rtre

Mhariri: Saumu Yusuf