1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia: Kiongozi wa upinzani awachiliwa huru

17 Januari 2018

Merera Gudina ameachiliwa huru Jumatano asubuhi baada ya kuwekwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka mmoja. Waandamanaji wa kabila kubw ala Oromos wamekuwa wakitaka aachiliwe huru

https://p.dw.com/p/2r2OI
Äthiopien Gudina Freilassung
Picha: DW/G. Tedla Hailegiorgis

Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Ethiopia cha Oromo Federalist Congress (OFC), Merera Gudina ameachiliwa huru Jumatano asubuhi baada ya kuwekwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kuachiliwa huru kwa Merera ndicho kitu kikubwa walichokuwa wakidai waandamanaji wa kundi kubwa la kikabila nchini humo la Oromos. Mnamo mwaka 2015, watu wa kabila la Oromo waliandamana dhidi ya pendekezo la kutaka kuupanua mji mkuu wa Addis Ababa. Wakihofia upanuzi huo utawapokonya ardhi yao .

Mamia waliuawa katika vurugu hizo, zilizosababisha kutangazwa  hali ya dharura iliyodumu miezi kumi na kumalizika mwezi Agosti. Merera ni kiongozi wa kwanza wa kisiasa kuachiliwa huru tokea Waziri Mkuu wa Ethiopia,  Hailemariam Desalegn, alipotangaza mapema mwezi huu kwamba wanasiasa wenye hatia watasamehewa.