1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eto'o asema Cameroon ina nafasi kubwa

9 Juni 2014

Cameroon walipambana vita vikali vya kufuzu lakini mwishoni wakajipa nafasi ya kushiriki kwa mara ya saba katika Kombe la Dunia. Na Indomitable Lions wako Brazil wakiwa na matarajio yenye majivuno.

https://p.dw.com/p/1CF46
Interaktiver WM-Check 2014 Mannschaft Kamerun
Picha: picture alliance/AP

“Kama tutafanya kazi ipasavyo, ili tunaweza kuanya vyema zaidi kuliko kilichofanywa na Ghana miaka mitatu iliyopita nchini Afrika Kusini”. Hayo ni maneno gwiji Samuel Eto'o. Hiyo itamaanisha kuwa waweze kufuzu katika nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya Ghana kufika robo fainali mwaka wa 2010. Eto'o aliisaidia Indomitable Lions kupata ushindi wa jumla ya magoli manne kwa moja dhidi ya Tunisia katika mechi za mchujo.

Kando na kufika katika robo fainali kwa usaidizi wa Roger Milla mwaka wa 1990, Cameroon wamepata ushindi mmoja pekee katika vinyang'anyiro vingine vitano na hawajawahi kuondoka katika awamu ya makundi. Haikuwa imefikiriwa kuwa Eto'o angeichezea tena Cameroon baada ya kutangaza kustaafu kutoka soka la kimataifa. Shirikisho la soka la Cameroon pia lilisitishwa na FIFA kwa madai ya serikali kuingilia masuala ya timu. Lakini adhabu hiyo iliondolewa wiki tatu baadaye. Kando na Eto'o kocha Mjerumani Volker Finke ana vipaji muhimu kikosini ikiwa ni pamoja na Eric Maxim Choupo-Moting, Pierre Webo, Nicolas N'Koulou, Alexandre Song na Jean Makoun.

Cameroon lazima wakuane na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico katika kundi A.

Mwandishi: Bruce Amani/dpa
Mhariri: Yusuf Saumu