1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EVORA: Vikosi vya Ulaya kulinda wakimbizi wa Darfur

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLk

Mawaziri wa ulinzi wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekusanya kikosi cha kama wanajeshi 2,000 kusaidia kuwalinda wakimbizi wa Darfur waliopo nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa,Herve Morin amesema,kiasi ya wanajeshi 1,500 wanatoka Ufaransa.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amesema kufuatia ahadi za wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya,hatimae ujumbe huo unaweza kupelekwa kama tume halisi ya Ulaya.Akaongezea kuwa Darfur ni maafa makubwa na ujumbe huo ni hatari.Mgogoro wa miaka minne na nusu katika jimbo la Darfur, magharibi ya Sudan umesababisha vifo 200,000 na zaidi ya watu milioni 2.5 wamelazimika kukimbia makwao.