1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

F1: Vettel anguruma mbio za Brazil

Bruce Amani
13 Novemba 2017

Mashindano ya Brazil yalihusu tu ni nani angeweza kuwa na mwanzo bora. Na ikabainika kuwa dereva wa Ferrari, Mjerumani Sebastian Vettel ndiye alianza vyema, na kumpiku dereva wa Mercedes Valtteri Bottas

https://p.dw.com/p/2nX5e
Formel 1 | Großer Preis von Brasilien | Sebastian Vettel jubelt
Picha: Reuters/P. Whitaker

Vettel alimpiku Bottas kwenye kona ya kwanza na akashikilia uongozi hadi mzunguko wa mwisho, ukiwa ni ushindi wa 47 wa taaluma yake, na wake wa tano msimu huu, na wake wa tatu nchini Brazil.

Ushindi huo uliimarisha udhibiti wa Vettel katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ubingwa wa dunia msimu huu, baada ya Muingereza Lewis Hamilton kunyakua taji hilo wiki mbili zilizopita mjini Mexico City. Jana, Hamilton alimaliza wa nne licha ya kuwa alianza katika mstari wa nyuma. Bottas alimaliza wa pili huku Kimi Raikkonen wa Ferrari akimaliza wa tatu

Dereva wa Brazil Felipe Massa alimaliza katika nafasi ya saba, na yalikuwa mashindano yake ya mwisho nchini Brazil. Atastaafu mashindano ya F1 katika wiki mbili zijazo. Kuondoka kwake kuna maana kuwa Brazil sasa haitakuwa na dereva wa F1 kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1969.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri:Moahammed Abdul-Rahman