1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA kuamua kuhusu rufaa ya Chelsea

Iddi Ssessanga
10 Aprili 2019

Shirikisho la kandanda duniani FIFA siku ya Alhamis litpitia rufaa iliyowasilisha na klabu ya Chelsea kupinga marufuku, ambayo kwa sasa inamaanisha haitaweza kusajili wachezaji wapya.

https://p.dw.com/p/3GYB0
Fußball Fans Chelsea v Southampton - FA Cup - Semi Final - Wembley Stadium
Picha: picture-alliance/Zumapress/R. Parker

Klabu hiyo ya The Blues ilipigwa marufuku kusajili wachezaji wapya wakati wa madirisha mawili yajayo ya uhamisho, baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja kanuni zinazohusiana na usaji wa watoto.

Chelsea ilikanusha kufanya makosa yoyote na mwishowe ikafungua shauri la rufaa na FIFA, ambalo litatathminiwa siku ya Alhamis (Aprili 11), ingawa uamuzi unaweza kuchukuwa wiki kadhaa.

Chelesea walistajabishwa na uamuzi wa kamati ya rufaa ya FIFA kutositisha vikwazo vyake wakisubiri kukamilika kwa mchakato wa rufaa.

Lengo, kwa mujibu wa duru za kuaminika, ni kutoa uamuzi "kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho la msimu wa joto" ili kuruhusu uwezekano wa klabu hiyo kuhamia kwenye mahakama ya utatuzi wa migogoro ya kimichezo, ikiwa rufaa yake itakataliwa.

Chelsea itasubiri kwa shauku uamuzi wa FIFA, hasa kwa sababu chini ya marufuku dhidi yake, klabu hiyo haitaweza kusaini mchezaji wa kuchukuwa nafasi ya mshambuliaji wa Kibelgiji, Eden Hazard, ambaye anatajwa kuwa mlengwa wa uhamisho wa kiasi cha euro milioni 116 kwenda real Madrid.

Chanzo: afpe