1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Finali ya kombe la dunia

19 Desemba 2008

Nani atatwaa kombe Manchester united au Quito ?

https://p.dw.com/p/GJpP
Paul Scholes, kati.Picha: AP

Kesho ni finali ya kombe la dunia la klabu bingwa huko Tokyo,Japan kati ya mabingwa wa Ulaya,Manchester United na La Liga de Quito ya Ecuador-kombe litaenda Uingereza kwa mara ya kwanza ?

Malkia wa mbio wa kenya bingwa wa olimpik wa mita 800 Pamela Jelimo,anyimwa nafasi ya kutwaa tena kitita cha dala milioni 1 na IAAF-shirikisho la riadha ulimwenguni katika mashindano ya mwakani na mzee Evander Holyfield,mbabe wa zamani wa wezani wa juu ulimwenguni arudi ringini-kisa nini ?

Tuanze na finali ya Kombe la dunia la klabu bingwa kati ya manchester United,mabingwa wa ulaya na Uingereza na Liga de Quito ya Ecuadaor:

Kabla ya finali ya kesho (jumapili)ya kukata na shoka,Sir Alex Ferguson,kocha wa Manchester united, aliwataka watoto wake kulipeleka kombe hilo Uingereza ili Manu iwe timu ya kwanza ya Uingereza kuvaa taji hilo. Manchester, mabingwa wa Ulaya, waliizaba Gamba Osaka ya Japan juzi alhamisi mabao 5-3 huko Yokohama na kutwaa tiketi yao kwa finali ya .

Quito ya Ecuador,iliotamba mbele ya mabingwa wa Mexico wanadai kombe litaenda Amerika ya kati na Manchester itapaswa kesho kuahirisha ndoto yake ya kuwa timu ya kwanza ya Uingereza kuigiza Bayern munich kuvaa tajila klabu bingwa ya dunia.

Wakati Manu iko Japan, wenzao Liverpool wanaongoza Ligi ya nyumbani .Kesho lakini, wanabidi kuitembelea Arsenal London kudai pointi 3.Mahasimu wao wakubwa Liverpool -Chelsea watakuwas uwanjani jumatatu wakiwa na miadi na Everton.

Ama katika Serie A-Ligi ya itali, Inter Milan kukibakia mpambano 1 kabla likizo ya x-masi na mwaka mpya, takriban ni viongozi wa Ligi mwaka huu 2008: Inter imefungua mwanya wa pointi 6 mbele ya maadui zao wakubwa Juventus turin.Inter ikiongozwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho, ina sasa jumla ya pointi 39 baada ya mechi 16.

Katika La Liga-ligi ya Spian, mabingwa Real Madrid wanacheza jioni hii na Valencia wakati Espanyol wako nyumbani wenyeji wa Atletico Madrid.Viongozi wa Ligi FC barcelona inayotamba na mkamerun samuel Eto-0 anaeongoza orodha ya watiaji magoli inarudi kesho uwanjani kupambana na FC Barcelona.

PAMELA JELIMO NA GOLDEN LEAGUE: IAAF imefuta mbio za mita 800 katika orodha yake ya mwakani ya mashindano ya miji 6 ya Golden League na hii itamuathiri bingwa wa mwaka huu-mkenya Pamela Jelimo:

Jane Nyingi anasimulia:

Malkia wa mbio za mita 800 wa Kenya aliegonga vichwa vya habari mwaka huu kwa kushinda medali ya dhahabu ya olimpik huko Beijing na baadae kushinda Jackpot-kile kitita cha dala milioni 1 katika mashindano mbali mbali ya Golden League, hatapata nafasi tena mwakani ya kutoroka na kitita kingine.

Shirika la riadha ulimwenguni-IAAF katika taarifa yake mwishoni mwa wiki hii limearifu kwamba katika mashindano ya 2009 mbio za mita 800 ambazo Jelimo ni bingwa wsa olimpik, hazitakuwamo katika orodha :Mwakani kutashindaniwa mbio za masafa ya mita 100 wanaume,mita 400,mita 3000,mita 5000 na mita 110 kuruka viunzi.Pia kuruka juu (High jump) na kwa upongoo (Pole vault.)

kitita cha dala milioni 1 huenda kwa mwanariadha atakaeshinda mashindano yake katika miji yote 6 inayoshindaniwa golden League.Jelimo ndie pekee aliefanya hivyo mwaka huu.Endapo hakuna mwanariadhaalieshinda mashindano yote mara 6,kitita hugawanywa kwa wale walioshinda mara 5.

Mashindano ya mwakani 2009 yanajumuisha yale mjini Berlin,Juni 14,Oslo July3,Roma July 10,Paris July 17,zurich August 28 na Brussels, Septemba 4.

Haiyumkiniki kwa bingwa mpya wsa rekodi ya dunia ya masafa ya mita 100,mjamaica Usain bolt,bingwa mara 3 wa Olimpik atapigania kitita hicho kwa kukimbia masafa ya mita 100,kwani wanariadha huchagua kwa uangalifu mkubwa ni mbio gani kukimbia ili waondoke na ushindi.

Kinyume na Jelimo,mcroatia Blanka Vlasic anaeruka High jump atapata nafasi nyengine ya kurekebisha makosa aliyofanya mwaka huu alipokosa ushindi 1 na Jelimo kumpiku.

Watakaoania pia kitita hicho cha golden League mwakani ni pamoja na malkia wa urusi wa Pole vault -Yelena IZINBAYEVA,mkuba Dayron Robeles ,bingwa wa olimpik na malkia wa mbio ndefu kutoka Ethiopia, Tirunesh Dibaba.

Haijulikani hata hivyo, ni wanariadha gani wsatashiriki mwakani katika Golden League,mwaka wa mashindano ya ubingwa wa riadha wa dunia mjini Berlin.

KUTOKA MEDANI YA RIADHA NA PAMELA JELIMO TUINGIE RINGI YA MABONDIA NA EVANDER HOLYFIELD:

Eric Ponda anasimulia:

Mbabe wa zamani wa wezani wa juu ulimwenguni aliewahi kutafunwa sikio na mbabe mwengine Mike Tyson, ameasmua kurudi leo ringini huko Zurich Uswisi kutwangana ndondi na Mrusi Nikolai VALUEV.

Jaribio hili la mbabe huyu wa zamani kutwaa taji la WBA limewagawa mashabiki wa ringi ya mabondia.Kuna wengine wanahisi wakati umewadia kwa mzee huyo kutoka kabisa ringini na kuanza kuwashughulikia watoto wake 11 katika qasri lake huko Atlanta, Georgia badala ya kujihatarisha kujeruhiwa ringini akiwa sasa na umri wa miaka 46.Kwani adui yake hataki mchezo,ameshindwa mara moja tu katika mapambano yake 50.

Jarida la New York Times limefika umbali wa hata kujiuliza: Je, "Holyfield ni shujaa au mwendawazimu?"

Evander mwenywe hajali ila hizo akidai bado ana mpambano mmoja mkali kuumaliza.

" Hayo wasemayo wengine, ni maoni yao."

Kwahivyo, ringi iwazi usiku wa leo huko zurich kupima rekodi yake Holyfield ya mapambano 53-akiwa ameshinda mara 42, ameshindwa mara 9 na sare mara 2. Ingawa ataondoka na kitita kati ya dala 600.000 na 750.000 kwa kumpa changamoto Valuev,Holyfield asingehitaji fedha hizo baada ya binafsi kuvuna jumla ya dala milioni 200 wakati wsa maisha yake ya miaka 20 ya mabondia.Alijipatia kitita cha dala milioni 35 kwa kutwangana tu na Mike Tyson. Holiyfield, alinukuliwa kutamba, "Ikiwa nina dala milioni 100 au dala milioni 200 mfukoni,ningeendelea hatahivyo kupigana."

Ushindi wa mwisho ringini wa Evander Holyfield ulikuwa miaka 8 iliopita alimtandika muamerika mwenzake John Ruiz kuvaa taji la WBA la wezani wa juu ulimwenguni na hivyo akawa bingwa wa dunia wa wezani huo kwa mara ya 4.

Tangu enzi hizo,Holyfield ameshindwa mapambano 11 na mara ya mwisho ilikuwa Oktoba mwaka jana alipodundwa na Sultan Ibragimov.

Azma ya Holyfield leo ni kuyaunganisha mataji ya WBA,IBF na WBC hadi mwisho wa mwaka ujao.Lakini kutamba mbele ya mrusi Valuev kutampa taji lake la 5 la dunia na kumfanya mbondia mkongwe kabisa kuvaa tena taji la wezani wa juu ulimwenguni.Hivyo angempiku mzee George Foremann aliefanya hivyo alipomtandika Michael Moore akiwa na umri wa miaka 45-mwaka mmoja kasoro na umri wa leo wa Evander Holyfield.Hii ilikuwa mwaka 1994.