1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREE TOWN:Kiongozi wa upinzani atangazwa kuwa rais

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBP0

Kiongozi wa upinzani nchini Sierra Leone Ernest Bai Koroma ametangazwa kuwa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi.

Tume ya uchaguzi nchini Sierra Leone imesema kwamba bwana Koroma wa chama cha All Peoples Congress ameshinda kwa asilimia 54.4 ya kura zote zilizohesabiwa.

Ernest Bai Koroma mwenye umri wa miaka 54 ameahidi kuleta mabadiliko nchini Sierra Leone.

Chama tawala cha Sierra Leonne Peoples Party kilijiandaa kuitaka mahakama kuu kuizuia tume ya uchaguzi kutangaza matokeo kikidai kwamba idadi ya wapiga kura ni kubwa mno kuliko ile iliyo andikishwa.

Lakini wasimamizi wa uchaguzi wamepongeza zoezi la kupiga kura katika awamu zote mbili na wamesema kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Takriban wapiga kura milioni 1.7 waliandikishwa katika daftari la wapiga kura.

Rais Ahmad Tejan Kabbah anang’atuka madarakani baada ya kukamilisha kipindi cha miaka kumi cha urais nchini Sierra Leone.