1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN : Wananchi wa Sierra Leone wapiga kura

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaM

Wananchi wa Sierra Leone leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa rais tokea wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo miaka miwili iliopita.

Ernest Bai Koroma wa chama cha upinzani cha All Peoples’ Congress APC anatazamiwa kutowa changamoto kali dhidi ya Solomon Berewa makamo wa rais wa nchi hiyo na mgombea wa chama tawala cha Siera Leones Peoples’ Party SLPP.

Rais Ahmed Tejan Kabbah ambaye alichaguliwa tena hapo mwaka 2002 kwa wimbi la furaha baada ya kipindi cha vita anan’gatuka kama inavyotaka katiba huku kukiwa na hasira ya wananchi juu ya rushwa iliokithiri na kushindwa kwa chama cha SLPP kutowa nafasi za ajira, umeme au kujenga barabara katika mojawapo ya nchi za kimaskini kabisa duniani.

Uchaguzi huu ni mtihani kwa taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo linarudi katika hali yake ya kawaida baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1991 hadi mwaka 2002.