1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN.Maafisa watatu wa kundi la waasi zamani wakutwa na hatia Serrileone

20 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBq0

Watu watatu wamekutikana hatia ya kuhusika na makosa ya uhalifu wa kivita pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya muongo mmoja nchini Sierreleone.

Hukumu hiyo ndiyo ya mwanzo kuwahi kutolewa na mahakama ya uhalifu wa kivita inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa nchini humo.

Watu hao Alex Tamba Brima, Brima Kamara na Santigie Borbor Kanu walikuwa maafisa wa ngazi ya juu katika kundi la waasi i walioiangusha serikali mwaka 1997.

Waasi hao inasemekana walikuwa wakiungwa mkono na rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor ambaye kwa sasa anasubiri kufikishwa tena mahakamani mjini The Hague katika kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili.

Wamekutikana na hatia ya makosa 12 kati ya 14.

Watatu hao wanakabiliwa na kifungo cha muda mrefu gerezani.Maelfu ya watu waliuwawa katika vita vya Sierreleone na waasi walibaka na kuwakata viungo raia wasiokuwa na hatia.