1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN:Viongozi wa waasi wapatikana na hatia

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpq

Viongozi wa zamani wa kijeshi nchini Sierra Leone wamepatikana na hatia na mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.Hii ni mara ya kwanza mahakama ya kimataifa inachukua hatua hiyo kuhusiana na utumiaji wa watoto katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea nchini Sierra Leone.Viongozi hao wa kijeshi wa zamani wanakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ugaidi,kutumia watoto kama wanajeshi,ubakaji,mauaji na utekaji.Kwa mujibu wa msemaji wa mahakama maalum ya Sierra Leone Peter Andersen,watu hao walifutiwa mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.

Mahakama ya Sierra Leone iliundwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika mwaka 2002.Watu 12 wameshtakiwa rasmi akiwemo rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor aliyehusika na kuwaunga mkono waasi wa Sierra Leone.