1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GARISSA:Ajali ya basi yasababisha vifo 16

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9l

Basi moja lililojaa abiria limepinduka na kubingiria zaidi ya mara tatu kaskazini mashariki nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu 17.Ajali hiyo ilitokea jana usiku mjini Garissa ulio na umbali wa kilomita 300 kutoka mji mkuu wa Nairobi.Polisi walilazimika kutumia tingatinga ili kulisogeza basi hilo waweze kuoka abiria walionasa.Kulingana na Antony Kibuchi mkuu wa polisi katika mkoa wa kaskazini,idadi ya abiria katika basi hilo ilipindukia.Hakuna maelezo zaidi kuhusu mkasa huo kwa sasa.