1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gates apokewa na mauaji Baghdad

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXi2

BAGHDAD.Watu 15 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari kulipuka katikati ya mji mkuu wa Iraq Baghdad.

Shambulizi hilo limetokea huku Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates akiwa mjini humo katika ziara ya kushtukiza na alikuwa akikutana na viongozi wa Iraq kwenye eneo lenye ulinzi mkali karibu na kulikotokea mlipuko huo.

Mapema kabla ya hapo watu watano waliuawa katika miji mingine kutokana na mashambulizi ya mabomu yaliyokuwa kwenye magari.

Hata hivyo pamoja na shambulizi hilo Waziri huyo wa Ulinzi wa Marekani alisema kuwa Iraq inakaribia kuwa katika hali ya utulivu na usalama.

Mjini Kabul watu 13 wameuawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga akiwa na gari lililojaa milipuko alipojibamiza katika basi la jeshi la Afghanistan.

Wanamgambo wa Kitaliban wamedai kuhusika na shambulizi hilo lililotokea kusini mwa mji huo mkuu hapo jana muda mfupi baada ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates kuhitimisha ziara yake ya ghafla na kuelekea Iraq.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Afghanistan General Mohammad Zahir Azimi amesema kuwa kati ya waliyouawa wanajeshi ni sita na raia saba.