1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gatlin atuma ujumbe kwa Bolt

10 Julai 2015

Mwanariadha wa Marekani Justin Gatlin amejiandaa kukutana na Usain Bolt na ameelezea matumaini yake kuwa Mjamaica huyo atakuwa katika hali nzuri kiafya katika mashindano ya uubingwa wa dunia mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/1Fwgk
Leichtathletik Justin Gatlin Sieger
Picha: picture alliance/dpa/J. Warnand

Gatlin, mwenye umri wa miaka 33, ataelekea katika mashindano ya riadha ya Beijing akiwa mmoja wa wanaopigiwa upatu kufanya vyema katika mbio za mita 100 na 200.

Wanariadha wengine wanaojiandaa kupambana na Bolt, ni Mjamaica Asafa Powell na Mmarekani Tyson Gay. Bolt atarejea mashindanoni katika Uwanja wa Olimpiki wa London kukimbia mbio za mita 100 katika mashindano ya Diamond League baadaye mwezi huu.

Tangazo hilo limekuja baada ya maumivu kwenye mguu wake wa kushoto kumfanya kujiondoa katika mashindano ya Paris mwezi uliopita na Lausanne Ahamisi wiki hii.

Bolt atashiriki mbio hizo za Julai 24, ikiwa ni miaka mitatu baada ya kushinda medali tatu za dhahabu katika Olimpiki, kwenye mbio za mita 100, 200 na mita mia moja wachezaji wanne kupokezana vijiti

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman