1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gauland wa AfD apinga wakimbizi Ujerumani

Sudi Mnette
23 Agosti 2017

Mgombea mkuu katika kinyang'anyiro hicho kwa tiketi ya Chama chenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia-Altenative for Germany,(AfD) Alexander Gauland ataka njia iliyo wazi katika kuwarejesha wakimbizi makwao.

https://p.dw.com/p/2igFb
Deutschland PK AfD "Bundeswehr in der Krise"
Mgombea ubunge wa tiketi ya chama cha AfD Alexander GaulandPicha: picture-alliance/dpa/B. Pedersen

Alexander Gauland ni mgombea mkuu wa AfD katika uchaguzi mkuu wa Septemba. Katika mahojiano yake na Mhariri Mkuu wa DW Ines Pohl na mwendeshaji  kipindi Jaafar Abdu-Karim, amesema  mipaka ya Ulaya pamoja na Ujerumani inapaswa kufungwa. Mwanachama huyo wa zamani wa chama cha kihafidhina cha Kansela Angela Merkel Christian Democratic Union, amesema kuwa ni makosa kwa watu wasioa na nyaraka zotote kuingia Ujerumani.

Nikimnukuu katika mahojiano yake hayo alisema" Watu hawa hawakupaswa, hata kuruhusiwa kuingia Ujerumani, na kuongeza waomba hifadhi wanapaswa kuwa katika vituo vya kuombea uhifadhi nje ya Ujerumani, au hata nje ya Ulaya, ambako wanaweza kuanza mchakato wao wa maombi kama watakuwa wanavigezo.

Amesema wale wote wanaokimbia vita katika maeneo kama Syria, wana haki ya kupata uhifadhi wenye kikomo kwa mujibu wa mkataba wa Geneva. Gauland anawania poamoja na Alice Weidel kama wagombea wenye siasa kali za mrengo wa kulia katika kinyang'anyiro cha ubunge. Gauland anasema ujerumani sio busati la dunia na kwamba taifa linavipaumbele vyake vya kuwajibika kwa wananchi na kwamba kupokea umma wa wakimbizi sio kipaumbele cha taifa kwa wakati huu. Anasema ni kweli kwamba idadi kubwa ya wakimbizi wanaingia Ujerumani kwa sababu za kiuchumi wakiwa na uhalali wa kutafuta maisha bora.

Wakimbizi waliamua kuingia Ujerumani kwa utashi wao

AfD Spitzenkandidaten Alice Weidel und Alexander Gauland
Wagombea Alice Weidel na Alexander GaulandPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Amesema ni jambo la kujtolewa wenyewe, hakuna aliwalazimisha kuingia Ujerumani kutoka maeneo ya Afrika kusini mwa jangwa la sahara au Libya kwa hivyo yeyote anaingia kwa kupitia Libya kwa namna yake mwenyewe anaweza vilevile kurudishwa atokako.

Chama cha AfD kilianza kujipatia umaarufu mkubwa tangu wakati wa kilele cha wimbi la wakimbizi mwaka 2015. Suala la wakimbizi ni moja kati ya suala muhimu kwa chama hicho kwa katika kampeni za uchaguzi wa 2017. Chama kina viti 13 katika nafasi za ubunge vya majimbo, kati ya majimbo 16 ya Ujerumani na inaweza kuingia katika bunge la shirikisho kwa mara ya kwanza katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 24. Uchunguzi wa maoni unaonesha kinaweza kupata asilimia 8 ya kura katika uchaguzi huo na kuwa na uwakilishi bungeni.

Gauland, ambae alijiondoa  kutoka chama cha Merkel cha  CDU mwaka 2013 baada ya kukitumikia  chama hicho kwa takribani muongo mmoja anasema sera zisizo na muongozo za wakimbizi za kansela Merkel zimekinufaika chama chake cha CDU. AfD inatofautiana katika mausala kadhaa na vyama vingine vya kisiasa nchini Ujerumani na sio CDU pekee. Tafauti mojawapo ni mbali na suala la wakimbizi , ni mada ya Uislamu, kukiwa na  waislamu takribani milioni tano nchini Ujerumani . Kiongozi huyo anasema Utamaduni wa Kiislamu na dini yenyewe kwa ujumla hauna nafasi nchini Ujerumani. Aidha pamoja na suala hilo vilevile kwa kuzingatia sera yao ya mambo ya nje AfD wanapinga vikali kitendo cha Urusi kujinyakulia eneo la Crimea.

Anasema kamwe Urusi haitolirejesha eneo hilo kwa mamlaka ya Ukraine lakini vilevile anafikiri kuwa vikwazo dhidi ya taifa hilo haviwezi kuwa na athari yoyote. Aidha Gauland anaipinga maombi ya Uturuki kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa kusema rais wa taifa hilo Recep Tayip Erdogan pamoja na kubakia  katika jumuiya ya kujihami ya NATO lakini anapaswa kujitenga na  sera za Ottoman mambo leo.

Mwandishi: Sudi Mnette/Abdul Karim DW
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman