1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Abbas na Olmert kujadili masuala ya usalama

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwt

Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas na Wazir Mkuu wa Israel Ehud Olmert wanatazamia kukutana juma lijalo,huku mapambano yakiendelea kwenye Ukanda wa Gaza.Pande zote mbili zimethibitisha kuwa mkutano huo utahusika na masuala ya usalama na juhudi za kuunda taifa huru la Palestina.Lakini Olmert alionyesha wasiwasi kuhusika na suala la kusitisha mapigano.Katika mashambulizi mapya kwenye Ukanda wa Gaza,wanajeshi wa Kiisraeli wamewaua wanachama 2 wa Hamas.Vile vile mbunge wa Kipalestina wa chama cha Fatah,Jamal Tirawi amekamatwa na vikosi vya Israel,kwenye Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.Hii ni mara ya kwanza kwa mwanachama wa Fatah alie mbunge wa Wapalestina kukamatwa na Israel.Sasa Israel imezuia zaidi ya wabunge 40 kutoka bunge la Wapalestina lenye viti 132.Wengi waliokamatwa ni wanachama wa Hamas.