1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza-Ban Kii Moon afanya ziara Gaza

Eric Kalume Ponda20 Januari 2009

Ni siku ya tatu leo tangu Israel ilipotangaza hatua ya kusimamisha mapigano katika eneo la Gaza , na hali ya utulivu bado inaendelea kushudiwa katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/Gca0
Mji wa Gaza uliobomolewa na wanajeshi wa Israel.Picha: AP

Wanajeshi wa Israel pia wanaendelea kuondoka katika eneo hilo huku maiti zaidi zikiendelea kufukuliwa kutoka vifusi vya majengo yaliyobomolewa wakati wa vita hivyo.


Hakuna milipo ya makombora wala maroketi iliyosikika katika eneo la Kusini mwa Israel na hali kadhalika mabomu kushambulia Gaza tangu hatua hiyo itangazwe siku ya Jumapili.

Mapigano yamemalizika ikiwa ni wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Israel tarehe 10 mwezi ujao, huku chama cha siasa za mrengo wa kulia cha waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu cha Likud na kile cha Leba cha waziri wa ulinzi Ehud Barak-vyote vikionekana kuwa usoni kwa mjujibu wa utafiti wa maoini ya wapiga kura.


Wakaazi wa eneo la Gaza wanaendelea kupekua vifusi na kuondoa maiti zaidi na kuifikisha idadi hiyo kuwa watu 1,310 na 5,500 wamejeruhiwa.


Serikali ya Israel imetangazwa kwamba inadhamiria kuwaondoa wanajeshi wake kutoka eneo hilo la Gaza kabla ya kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Baraka Obama baadaye leo jioni, ingawa bado kunataarifa ya kutatanisha kwamba Israel inataka kuwabakisha sehemu ya wanajeshi wake ndani ya Gaza. Tayari wanajeshi wa akiba walioingia Gaza wameondoka na kuachiliwa kuendelea na shughuli zao za kawaida.


Katibu mkuuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kii Moon pia anatarajiwa kuzuru eneo la Gaza ikiwa hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa ngazi za juu kutembelea eneo hilo tangu mashambulio hayo yaanze.


Katibu mkuu huyo alisisitiza alipofanya mazungumzo na maafisa wa serikali nkwamba ziara yake ni kukadiria athari zilisababishwa na vita hivyo vilivyodumu kwa muda wa siku 22 na misaada ya kibinadamu inayohitajika kwa wakaazi wa Gaza.


Bw Ban Kii Moon anatarajiwa kusafiri kwa ndege ya kijeshi ya Israel hadi eneo la mpakani la Erez kabla kuingia Gaza.


Wakati huo huo Mkuu wa shirika la Afya Duniani Margaret Chan amesema mjini Geneva kwamba eneo hilo la Gaza linakabiliwa na hali ngumu ya ukosefu wa huduma za Afya na kwamba wakaazi wake wanakabiliwa na tisho la magonjwa. Chan alisikitishwa na hatua ya Israel ya kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza .






Eric Ponda / Reuters.