1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza-Baraza Umoja wam mataifa lapitisha azimio.

Eric Kalume Ponda12 Januari 2009

Baraza la kutetea haki za binadamu la Umoja wa mataifa liliogawanyika limepitisha azimio kuishtumu Israel kuendeleza mashambulizi katika ukanda wa Gaza na kuishtumu kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/GWlR
Wanajeshi wa Israel wanaouzingira mji wa Gaza.Picha: AP


Hayo yamejiri huku Israel ikisimamisha kwa muda wa masaa matatu mashambulizi yake ili kutoa nafasi ya misaada ya kibinadamu kupelekwa katika eneo hilo.


Hata hivyo kabla ya kuanza kutekelezwa kwa usmamishaji wa mashambulio hayo wanajeshi wa Israel walifanya mashambulizi makali karibu na makao makuu ya kiongozi wa chama cha Hamas katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza.


Azimio hilo linalohimiza kuundwa kwa kamati maalum kuchunguza visa vya ukiuakaji wa haki za binadamu vinavyotekelezwa na wanajeshi wa Israel dhidi ya Wapelestina katika vita hivyo, lilipitishwa baada ya kuzuka mgawanyiko mkubwa baina ya Matiafa ya magharibi na yale ya Kiarabu, Africa ,Asia na Marekani Kusini.


Wajumbe 33 walipiga kura kuunga mkono azimio hilo lililopingwa vikali na mataifa 13 wanachama hasa kutoka mataifa ya magharibi ambayo yalisita kupiga kura isipokuwa Canada.


Sababu zilizotolewa na mataifa ya magharibi wakati wa kupitishwa kwa azimio hilo ni kwamba linaegemea zaidi upande wa Wapalestina na kupuuza mashambulizi ya makombora ya maroketi dhidi ya Israel.


Kamishna mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja huo Navi Pillay, alisema kuwa Israel imetekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuwashambulia maafisa wa huduma za kibinadamu katika eneo hilo mbali na kupuuza azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa.


Huku hayo yakijiri Wanajeshi wa Israel watekeleza mashsambulizi makali karibu na makao ya kiongozi wa chama cha Hamas katika ukanda huo wa Gaza kabla ya kuanza kutekeleza tena mpango wa kusitisha mapigano kwa muda wa masaa 3 ili kutoa nafasi ya huduma za binadamu kufika Gaza.


Watu 7 waliuawa wakiwemo wanawake 2 na watoto wawili wakati wanajeshi wa Israel walipofanya mashambulizi hayo katika miji ya Sheikh Anjleen, Tal el-Hawa, Zaytoun, hejaeya na Al-Tufa.


Mashambulizi hayo yameendelea baada ya Israel kuwapeleka wanajeshi zaidi wa akiba ambapo sasa yaripotiwa wanalikaribia eneo la Gaza lenye idadi kubwa ya watu huku Israel ikiendelea kupuuza wito wa jamii ya kimataifa kukomesha mapigano hayo huku msemaji wa serikali Mark Regev akisisitiza kuwa ni Israel pekee itakayoamua lini kukomesha mashambulizi hayo


Hata hivyo mjumbe maalum katika eneo hilo la mashariki ya kati waziri mkuu wa zamani wa Uingezera Tonny Blair ambayo yuko mjini Cairo, alisema kuwa utaratibu wa kusitisha mapigano kupitia mpango wa amani unaoongozwa na Misri unakaribia kukamilika na kunamatumaini makubwa ya kukomeshwa kwa vita hivyo.


Alisema haya baada ya kushauriana na kiongozi wa mpango huo Rais Honsi Mubarak kwamba mashaurianao hayo yamefika awamu muhimu alisema Tony Blair ``Tumeeleza masikitiko yetu kwa kila mmoja wao, kwasababu tunataka azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa litekelezwe. Pande yote mbili Hamas na Israel zinafahamu kinachohitajika kufanywa kukomesha mzozo huu. Hamas wakomeshe mashambulizi ya maroketi na kukubali mpango wa kuzuia uingizaji silaha kimagendo kupitia maeneo ya mpakani ndipo maeneo haya yatakapofunguliwa kuambatana na maazimio ya kimataifa yaliyofikiwa miaka 3 iliyopita kuhusiana na vivuko hivyo vya mpakani´´.


Kuna habari kuwa ujumbe wa chama cha Hamas unaohudhuria mashauriano hayo hata hivyo ulikataa baadhi ya vipengee kwenye mapendekezo hayo ya kukomeshwa mapigano ili kutoa tu nafasi ya misaada ya kibinadamu kwa raia wa Gaza.


Mashauriano hayo yanayoingia siku yake ya pili hivi leo, bado yamesusiwa na mjumbe wa Israel Amos Gilad ambaye alichelewesha ziara yake mjini Cairo akisubiri matokeo ya kikao cha baraza la usalama nchini Israel.



Misri imesema kwenye mapendekezo hayo kwamba iko tayari kuwaruhusu wachunguzi kukagua mizigo inayopitishwa kwenye mpaka wake na Gaza na kwamba Israel inapasa kufungua maeneo ya mpakani.


Hata hivyo serikali hiyo ya Misri imekataa pendekezo la kufungua eneo la mkapani la Rafa kama ilivyoüpenfdekezwa kwenye mkataba uliofikiwa mwaka wa 2005.


Zaidi ya Wapelstina 900 wameuawa na zaidi ya 3,000 kujeruhiwa tangu vita hivyo vianze disemba 27. Isarael pia imewapoteza wanajeshi wake 11 na raia 3 kwenye vita hivyo.