1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY: Bunge la Wapalestina kuidhinisha serikali mpya

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCI4

Wabunge wa Kipalestina wanakutana mjini Gaza kuidhinisha serikali mpya ya umoja wa kitaifa baada ya kuwepo mapambano makali kwa majuma kadhaa kati ya makundi hasimu Hamas na Fatah. Waziri Mkuu mteule,Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas amesema,baraza lake la mawaziri litajitahidi kuendeleza makubaliano ya kuweka chini silaha pamoja na Israel.Wakati huo huo amesema,hatua za kupinga uvamizi wa Israel katika maeneo ya Kipalestina ni halali.Kwa upande mwingine,Rais Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah, katika hotuba yake bungeni,ametoa wito wa kujadialiana na Israel kutafuta suluhisho la amani na kuachilia mbali matumizi ya nguvu ya kila aina.Israel kwa upande wake,imekataa kabisa kujadiliana na serikali ya Wapalestina iliyopendekezwa,ikisema kuwa chama cha Hamas kimepinga masharti ya kuacha matumizi ya nguvu na kulitambua taifa la Kiyahudi.Kikao cha bunge la Wapalestina mjini Gaza,kimehudhuriwa na wabunge 87 kutoka jumla ya 132.Wengi wengine wapo katika jela za Israel.