1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Israel yawauwa wapiganaji wawili wa chama cha Hamas huko Gaza

21 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqt

Taarifa kutoka ukanda wa Gaza zinasema kuwa Israeli imeshambulia kwa kombora na kuwauwa wanaharakati wawili wa kipalestina wakati wakiwa ndani ya gari lao mashariki mwa mji wa Gaza. Mashahidi wanasema watu 6 wakiwemo watoto 2 waliokuwa karibu na barabara kulikofanyika shambulio hilo la kuvizia, wamejeruhiwa. Chama tawala cha Hamas kimesema watu hao wawili waliouawa walikuwa ni wapiganaji wa tawi lake la kijeshi la al-Qassam Brigades. Israel imesema imelilenga gari lilokuwa likibeba watu ambao imewataja kuwa ni magaidi.

Mashambulizi hayo ya Israel yameendelea wakati mazungumzo kwa ajili ya kuunda serikali ya umoja wa taifa katika maeneo ya wapalestina yamekwama. Makundi hasimu yameshindwa kufikia maridhiano juu ya ugavi wa wizara muhimu. Kwa muda wa miezi kadhaa sasa, rais Mahmud Abbas, amekuwa akijaribu kuunda serikali ya mseto kwa lengo la kuzishawishi nchi zenye nguvu kama Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya kuviondoa vikwazo vilivyowekewa chama cha Hamas.