1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza : Makubaliano mapya ya kusimamisha mapigano Gaza

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChk

Majeshi ya usalama ya Palestina yameanza kuyahama baadhi ya maeneo ya mji wa Gaza na kuwaachia huru watu waliotekwa nyara, katika mapigano ya karibuni kati ya wapiganaji wa Hamas na Fatah. Hatua hiyo inatokana na kufikiwa makubaliano mapya ya kusimamisha mapigano. Waziri mkuu Ismail Haniya alitoa wito hapo mapema akiwataka Wapalestina kuwa na umoja, baada ya mapigano makali ya risasi mjini Gaza kati ya pande hizo mbili. Wanaharakati sita waliuwawa jana. Makubaliano ya kusimamisha mapigano yamefikiwa baada ya upatanishi ulioongozwa na Misri.