1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mashambulio ya Israel yaendelea Ukanda wa Gaza

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0g

Ukanda wa Gaza umeshambuliwa tena na vikosi vya anga vya Israel.Ripoti zinasema jumla ya watu 10 waliuawa katika uvamizi huo wa angani,Israel ikisema mashambulio matano yalilenga makao makuu ya chama cha Hamas.Tangu siku ya Jumatano,Israel imefanya mashambulio 13 katika Ukanda wa Gaza,baada ya wanamgambo kuvurumisha makombora kusini mwa Israel.Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas ametoa mwito kwa Marekani kusitisha mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel.