1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Mawaziri wa Hamas kususia hotuba ya rais.

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiw

Baraza la mawaziri la serikali inayoongozwa na chama cha Hams limesema linapanga kususia hotuba leo Jumamosi itakayotolewa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas ambapo anatarajiwa kuitisha uchaguzi na mapema. Hii inakuja kutokana na hali ya ghasia inayoendelea kati ya waungaji mkono wa chama cha Hamas na mahasimu wao wa majeshi yanayomuunga mkono rais Abbas katika ukingo wa magharibi na Gaza. Katika mkutano uliohudhuriwa na wafuasi wapatao 100,000 wa chama cha Hamas , waziri mkuu Ismail haniyeh ametoa wito wa umoja wa kitaifa kwa manufaa ya kuikomboa Palestina. Kiasi watu 30 wamejeruhiwa katika mapigano ya hivi karibuni ambapo yalikuja siku moja baada ya watu wenye silaha kufyatua risasi dhidi ya ujumbe wa waziri mkuu Haniyeh katika kivuko cha mpakani cha Rafah, na kumuua mlinzi mmoja. Hamas imesema kuwa shambulio hilo lilipangwa kwa makusudi kutaka kumuua waziri mkuu Haniyeh.