1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA. mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa yagonga mwamba

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqx

Kamishna wa maswala ya haki za binadamu wa umoja wa mataifa Louise Arbour ameanza ziara yake katika maeneo ya Israel na Palestina licha ya kwamba eneo hilo linakabiliwa na mashambulio mapya.

Kamishna huyo amewahakikishia watu wa palestina kwamba ulimwengu bado haujawa telekeza.

Bibi Arbour yuko katikamziara ya siku tano na anatarajiwa kukutana na viongozi wa Israel na Palestina pamoja na kuzuru maeneo yaliyoathirika katika machafuko ya hivi karibuni.

Louise Arbour amezuru maeneo ya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ambako jamii ya watu 19 iliuwawa mapema mwezi huu katika shambulio lililotekelezwa na majeshi ya Israel.

Wakati huo huo mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja kati ya chama cha Hamas kinachotawala mamlaka ya Palestina na chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas yamegonga mwamba na kuzorotesha juhudi ya kumaliza mgomo wa misaada dhidi ya serikali ya Hamas unaofanywa na jamii ya kimataifa.