1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wafuasi wa Fatah walipiza kisasi Ukingo wa Magharibi

16 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBr9

Mamia ya wafuasi wa chama cha Fatah waliobeba silaha,wamevamia taasisi zinazoongozwa na chama cha Hamas kwenye Ukingo wa Magharibi.Miongoni mwa majengo yaliyovamiwa ni bunge na wizara za serikali.Wafuasi hao wa Fatah wamesema,yeyote anaehusika na Hamas hatoruhusiwa kurejea.Hayo yametokea siku moja baada ya chama cha Hamas kuuteka Ukanda wa Gaza kufuatia mapambano makali. Mjini Gaza,wanachama wa Hamas wamepora nyumba ya aliekuwa rais wa Wapalestina,marehemu Yasser Arafat.Kwa upande mwingine,vikosi vya Kiisraeli kwenye kituo cha mpakani kati ya Erez na Gaza,vimefyatua risasi kuwaonya Wapalestina wapatao dazeni kadhaa,ambao walijaribu kukimbia mapigano.Wakati huo huo,Salam Fayyad alieteuliwa kama waziri mkuu mpya wa Wapalestina,anatazamia kulitangaza baraza lake la mawaziri siku ya Jumapili.Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas amemchagua Fayyad mwanasiasa huru aliekuwa waziri wa fedha,baada ya kumfukuza Waziri Mkuu Ismail Haniyeh wa Hamas,hatua ambayo chama cha Hamas kinasema si halali.