1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wanamgambo wa Hamas na Fatah wapambana upya

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVr
waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown
waziri mkuu wa Uingereza Gordon BrownPicha: AP

Mapigano makali yamezuka kati ya wanamgambo wa Hamas na Fatah,kwenye chuo kikuu cha Kiislamu mjini Gaza.Mapambano hayo mapya yanahatarisha mapatano ya kuweka chini silaha yaliokubaliwa na makundi hayo hasimu siku ya Jumanne.Ripoti zinasema,wanamgambo wanaokiunga mkono chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas,walikivamia chuo kikuu cha Kiislamu ambacho ni ngome ya Hamas.Vyombo vya habari vinasema,idadi fulani ya Wairani walio wataalamu wa silaha,walikamatwa na kwamba Muirani mmoja alijiua.Vile vile siku ya Alkhamisi,hadi Wapalestina 6 waliuawa katika mapigano yaliyozuka kati ya Hamas na Fatah kwenye Ukanda wa Gaza.