1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Abbas ailaumu Israel

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnp

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameilaumu Israel kwa uvamizi iliyoufanya huko ukanda wa Gaza na ukingo wa Magharibi na kusema kuwa huo ni uhalifu.

Majeshi ya Israel yakiwa na vifaru na magari ya deraya hapo jana yalivamia maeneo hayo ambapo wapalestina tisa waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Shutuma hizo za Rais Abbas zinakuja huku kukiwa na habari kuwa huenda Tonny Blair akateuliwa kuwa mjumbe maalum huko mashariki ya kati.

Serikali ya Palestina imesema kuwa ina matumaini na Blair iwapo atapewa nafasi hiyo.