1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA.Hali ya usalama yaimarika licha ya ghasia za hapa na pale

30 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWX

Hali ya usalama inazidi kuimarika katika maeneo ya Palestina licha ya kuzuka ghasia hapo jana usiku baada ya makundi ya Hamas na Fatah kuafikiana kusimamisha mapigano.

Makubaliano hayo ya kusimamisha mapigano yaliafikiwa kati ya waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniya wa chama kinacho tawala cha Hamas na muwakilishi wa rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas hapo jana katika juhudi za kuzuia machafuko zaidi katika maeneo ya Palestina.

Ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea katika maeneo ya Palestina zilianza siku ya alhamisi iliyopita na kusabbaisha vifo vya watu 30.

Maduka na shule yalilazimika kufungwa kwa muda wa siku tano kufuatia machafuko kati ya makundi ya Hamas na Fatah.