1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Wapalestina tisa wauawa

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMK

Majeshi ya Israel yamewaua wapalestina tisa katika mashambulizi mawili tofauti kwenye ukanda wa Gaza na kutishia kuendelea zaidi na mashambulizi hayo ikiwa ni kulipiza kisasi kutokana na mashambulizi ya maroketi kutoka kwa wanamgambo wa kipalestina.

Katika shambulizi moja, kombora la Israel lililipiga gari na kuwaua wapiganaji watano wa kipalestina.

Katika mji wa Beit Hanun mashuhuda wanasema kuwa mtu mmoja aliyekuwa na bunduki na wengine watatu waliuawa baada ya majeshi ya Israel kuvamia eneo hilo.

Hiyo ni baada ya makombora 12 kufyatuliwa na wanamgambo wa kipalestina dhidi ya mji wa kusini mwa Israel wa Sderot.